<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><lyrics>[V1]
 Nitaimba ya Yesu,
 Kwa rehema zake,
 Baraka nyingi sana
 Nimepata kwake;
 Nitaimba ya Yesu,
 Sadaka ya Mungu,
 Alimwaga damu
 Ukombozi wangu.

[V2]
 Nitaimba ya Yesu
 Hapa siku zote,
 Nitakapokumbuka
 Vyema vyake vyote;
 Nitaimba ya Yesu
 Hata mashakani,
 Yeye atanilinda
 Mwake ubavuni.

[V3]
 Nitaimba ya Yesu
 Niwapo Njiani;
 Takaza Mwendo, hata
 Nifike Mbinguni;
 Nikiisha ingia
 Mlangoni mle,
 Yesu nitamwimbia
 Mbinguni milele.</lyrics>
<title>Nitaimba Ya Yesu TZR109</title>
<hymn_number>109</hymn_number>
</song>